Timu ya kilinux inayofuraha kuwatangaza kuwa Jambo Mozilla Firefox 1.o.3,
toleo la Kiswahili la Mozilla Firefox 1.0.3, ipo tayari kwa mapakuzi. Programu hii
inapatikana katika matoleo mawili; moja kwa ajili ya kompyuta zenye na mfumo wa
Windows XP na jingine kwa ajili ya kompyuta za Linux. Kupakua jambo Mozilla Firefox
nenda kwenye kipengele cha mapakuzi (kwenye tovuti hii) na chagua Pata Mozilla Firefox.
| Mradi wa KiLiNuX ulitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mashindano ya Stockholm 2006 baada ya kuwa mradi bora wa TEKNOHAMA katika kategoria ya Elimu kwenye mashindano hayo. Jumla ya miradi 172 kutoka mataifa mbalimbali ilichuana ambapo miradi 32 tu ndio ilifanikiwa kuingia fainali. | ![]() | ||||||
| Baraza la Mashindano la Stockholmlimeupitisha Mradi wa Kilinux kama moja ya miradi iliyoingia fainali katika kategoria ya Elimu kwa tuzo za mwaka huu za Mashindano ya Stockholm. Miradi 148 imetangazwa kuwa imeingia fainali za mashindano hayo yenye kategoria sita ambazo ni Utamaduni, Maendeleo ya Uchumi, Elimu, Mazingira, Afya na Utawala wa umma. Mshindi wa kila Kategoria atatangazwa wakati wa maadhimisho ya kukabidhi zawadi jijini Stockholm Mei 11. |
![]() | ||||||
Timu ya kilinux ilihudhuria mafunzo ya ujanibishaji yaliyofanyika Afrika
ya Kusini kuanzia Novemba 28, 2005 hadi Desemba 2, 2005. Mafunzo haya
yaliandaliwa kwa pamoja na Translate.org.za (Mradi wa Ujanibishaji wa
Afrika Kusini) na Kilinux.udsm.ac.tz (Mradi wa Ujanibishaji wa Tanzania).
Madhumuni hasa ya mafunzo haya yalikuwa ni kutoa mafunzo kwa timu ya
Kilinux juu ya utaalamu wa kiufundi na kilugha unaohitajika kwa ajili
ya mchakato wa ujanibishaji. Mafunzo yaliongozwa na wafanyakazi
wa Translate.org.za.
Timu ya Kilinux ilijifunza mambo yafuatayo:
Mradi wa Kilinux ulikua ni mojawapo ya miradi iliyoshiriki katika Kilele cha
Mkutano wa Dunia wa Jamii ya Habari (WSIS) uliofanyika Tunis, kuanzia
Novemba 16 hadi Novemba 18, 2005. Mkutano huo ulikusanya wawakilishi
kutoka miradi mbalimbali na waanzilishi wengineo kutoka duniani kote.
Mojawapo ya malengo ya Kilele hiki ni kuunda Jamii ya Habari madhubuti ili
watu kila mahali waweze kuunda, kufikia na kuchangia habari na maarifa ili
kufanikisha na kutimiza shabaha na malengo ya maendeleo yaliyokubaliwa.
Kilele hiki kinatazamwa kama msingi muhimu katika jitihada za dunia kuondoa
umaskini. Vilevile kimetoa utambuzi juu ya faida ambazo Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEKNOHAMA) inaweza ikaleta kwa jamii na jinsi ya
kubadilisha kazi, mawasiliano na maisha ya watu.
Kwa ukweli huo, mikutano na midahalo mingi ilifanyika ili kujadili na kuchangia
mawazo na maarifa kuhusu jinsi gani ya kufanikisha shabaha na malengo
yaliyokubaliwa. Mwakilishi wa Mradi wa Kilinux alipata nafasi ya kuwasilisha
mada juu ya kilinux na mchakato mzima wa ujanibishaji programu huria
Novemba 17 siku ambayo ilifahamika kama Siku ya Tanzania. Uwasilishaji
huo ulifuatiwa na maswali.
Kwenye banda la Tanzania programu ya Jambo OpenOffice na Jambo Mozilla
Firefox zilioneshwa, na watu wengi walivutiwa sana na programu hizi.
Baadhi ya watu waliovutiwa na klnX na wakapewa nakala ya CD ya
Jambo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Astrid Dufborg balozi wa
TEKNOHAMA kwa Sweden na mkuu wa ujumbe wa Sweden WSIS,
Mhe. Nandi-Ndaitwah waziri wa Habari na Utangazaji wa Namibia,
Mhe. Dk Ivy Matsepe-Casaburri waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini
na mabalozi wetu Ami Mpungwe na Mohammed Sheya na wengine wengi.
Picha za baadhi ya matukio zitakuwepo baada ya muda.
Sasa hivi tupo katika mchakato wa kusajili ili kupata akaunti ya CVS kwa ajili
ya ujanibishaji wa Firefox kutoka shirika la Mozilla. Hili litachukua siku kadhaa
kupata ufikio kwenye seva ya CVS.
Timu ya klnX ipo mbioni kuanza uhamishaji wa Jambo OpenOffice kutoka toleo 1.1.3 kwenda toleo 2.0
kwa kushirikiana na Alberto Escudero kutoka it46 Global Consultancy.
Kulingana na mpangilio wa sasa wa kazi, mchakato wa uhamishaji unatarajiwa kukamilika Januari 2006.
Timu imeshakusanya zana zote muhimu kwa ajili ya mchakato wa uhamishaji. Baada ya kuunganisha Jambo
OpenOffice 1.1.3 na OpenOffice 2.0, tulipata jumla ya tungo 57844 kati ya hizo takribani tungo 20000
zimetafsiriwa.
Bado tunashughulikia kisakinishi cha firefox 1.0.3 kwa ajili ya Linux na Windows XP. Kisakinishi cha
Linux karibia kinakamilika ingawa majaribio yameonesha kuwa kimeshindwa kusakinisha katika baadhi ya
kompyuta hivyo timu bado inaendelea kurekebisha tatizo hili.
Katika Maonesho ya 29 Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam Timu ya Kilinux ilipata
fursa ya kuonesha toleo la kwanza la Kiswahili la OpenOffice.org 1.1.3 liitwalo Jambo.
Watu wengi kutoka nje na ndani ya Tanzania wanashangaa waonapo program hii na kuthamini
juhudi za timu ya Kilinux katika uswahilishaji wa Programu Huria. Wengi wao waliichukua
programu na wengine walichukua anuani ya tovuti ili waende kupakua Jambo OpenOffice moja
kwa moja kutoka kwenye mtandao.
Watu walivutiwa sana kutumia programu hii mpya kwasababu si kwamba itarahisisha kazi
zao tu bali pia itapunguza muda wa kuzifanya kazi hizo. Kazi zitafanyika kwa ufanisi
zaidi hususani shughuli za kuandaa maandiko, mawasilisho, ripoti, michoro n.k. katika
lugha ya Kiswahili ambayo ni muhimu sana Afrika ya Mashariki na Kati na sehemu
nyingine ulimwenguni. Watu walielewa pia faida za kutumia Programu Huria kulinganisha
na Programu funge. Wengi wao walikua hawazifahamu Programu Huria. Waliahidi kuja
idara ya Sayansi ya Kompyuta kujionea nini kinaendelea na kuchukua programu hii.
Watu wengine kutoka Afrika ya Mashariki na Kati wameshachukua programu hii,
watu kutoka Ulaya mathalani Ujerumani, Ubeligiji n.k. na Marekani walisema wanatumia
sasa hivi Jambo OpenOffice nchini mwao. Timu ya Kilinux inawashukuru kwa kukubali
programu za Kiswahili na inaahidi kuendelea na mchakato wa uswahilishaji mpaka mfumo
kamili wa uendeshaji kwa Kiswahili utakapotokea.
Katika maonesho ya programu, machapisho na vitabu mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es salaam yaliyofanyika Dodoma (Bungeni), Timu ya Kilinux ilipata fursa ya kuonesha
programu ya kwanza ya kiswahili iitwayo Jambo OpenOffice.org 1.1.3 ambayo humuwezesha
mtumiaji wa lugha ya Kiswahili kuunda maandiko, mawasilisho, michoro, kuunda tovuti n.k.
Katika Maonesho hayo waheshimiwa mawaziri na wabunge walikipongeza chuo kikuu cha
Dar es Salaam kupitia idara ya Sayansi ya Kompyuta kwa kuanzisha mradi wa Uswahilishaji
Programu Huria. Pia walichukua programu hiyo kwa wingi ili ikatumike maofisini na sehemu
nyinginezo nchini.
Tamko la Casablanca
Wataalamu wa ujanibishaji wa Afrika walikutana Casablanca kwenye warsha iliyoandaliwa na shirika
lisilo la kiserikali la Kabissa ikigharamiwa na IDRC, kwa ushirikiano na Technopark Centre.
Tukio lilinufaika kutokana na uchangiaji kutoka kwa Waziri wa Teknolojia ya Habari wa Morocco,
Balozi wa Canada na wataalamu kutoka mabara mengine. Baada ya siku tatu za kazi, washiriki wa
mkutano walifikia mahitimisho yafuatayo:
Uzuiaji watu katika matumizi ya teknolojia ya habari na masiliano (TEKNOHAMA) kwa lugha ya kigeni
kunazidisha mgawanyiko wa kidigiti; hufanya uchukuaji/utumiaji wa TEKNOHAMA kuwa mrefu,
mgumu, na wa gharama; na hufukarisha tamaduni kaya.
Ujanibishaji unafanya TEKNOHAMA iwe inafikiwa zaidi na kila mtu, ukijumuisha watumiaji kutoka
vijijini na wanafunzi wachanga, ukiimarisha umuhimu wa utamaduni wetu na kutusaidia kuhifadhi
utambulisho wetu. Ujanibishaji wa TEKNOHAMA kwenda lugha za asili za Kiafrika hivyo ni ufunguo
wa maendeleo ya haraka na haki Afrika. Ili ujanibishaji ufanikiwe na uwe na matokeo ya juu
kwenye jamii, ushirikiano kati ya serikali, jamii, waelimishaji, wana isimu, wataalamu wa
wa kompyuta, mashirika sadifu na wafadhili ni muhimu.
Sisi, washiriki, tunaahidi kusimamia/kukuza mtazamo huu na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo
ya jamii Afrika kupitia ujanibishaji wa TEKNOHAMA.
Timu ya klnX ipo mbioni kukamilisha uswahilishaji wa firefox-1.0.3.
Timu ina furaha kutangaza uundaji wa kwanza wa kivinjari webu cha firefox kwa Kiswahili.
Bado tunaendelea kuiboresha programu hii na kuondoa hitilafu ndogondogo ambazo zimejitokeza.
Pongezi kubwa kwa wana klnX wote.

Sasa hivi tunaunda toleo la Kiswahili la tovuti ya kilinux.
Kwahiyo, tovuti yetu itakuwa inapatikana katika lugha mbili (Kingereza & Kiswahili).
Kwa sasa kurasa nyingi za toleo la Kiswahili bado zimeandikwa kwa kingereza
au lugha zote mbili. Ila tunatarajia kutoa toleo kamili la Kiswahili hivi punde.
Tovuti rasmi ya kilinux sasa ni http://www.kilinux.udsm.ac.tz, tovuti
ya awali http://www.kilinux.org haitumiki tena. Hivyo, taarifa zote kuhusu
mradi huu na maendeleo yake zitakuwa zinapatikana kwenye tovuti hii. Mapakuzi ya
Jambo OpenOffice.org 1.1.3 sasa yanapatikana kwenye kipengele mapakuzi katika
tovuti hii rasmi ya kilinux badala ya http://www.o.ne.tz.
Mradi wa Kuswahilisha Programu Huria (Kilinux) una furaha kutangaza uzinduzi rasmi wa Jambo OpenOffice.org utakaofanyika tarehe 28 Februari 2005. Uzinduzi rasmi wa toleo la Win32 la Jambo OpenOffice utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Dar es Salaam (Tanzania).
Tukio hilo litahudhuriwa na balozi Tolvald Akesson (Balozi wa Sweden, Tanzania) na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Frederick Sumaye na Mhe. Pius Ng'wandu (Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu).
Uzinduzi Rasmi wa Jambo OpenOffice.org
Mahali: Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Dar es Salaam
Tarehe: Februari 28, 2005
Muda: 3:30 UM - 6:00 MU
Kiingilio: Bure
We are preparing the release of Jambo OpenOffice.org and need some mirrors (Specially in Tanzania and East Africa). The size of the software is as follows:
Contact kenny@cs.udsm.ac.tz if you can offer some collocation space for the software.
We are getting ready...
As announced we are preparing the release of Jambo OpenOffice for MS Windows and Linux. The release CD will contain the following software:
Mirror sites: If you are interested in having a mirror of the CD in a ISP in East Africa, contact Alberto Escudero-Pascual aep@it46.se
To download the latest version check the Download section http://www.o.ne.tz/download.php



More info and download here.
As the Father of Tanzania, the late Mwalimu Nyerere will always be
remembered by his famous saying: "It can be done; play your part".
Today, 4th December 2004, The Open Swahili Localization Project, also
known as Kilinux, is proud to announce the first ever release of a
free office suite software in Swahili, called "Jambo OpenOffice."
A full coverage of the release in six languages is now available in the website: http://oo.o.ne.tz
Completed 2395 out of 3036 S-Writer strings (80%)
Completed 12762 out of 18080 strings (70%)
Completed 93 out of 174 .PO files (53%)
Completed 7165 out of 14044 unique strings (51%)
Note about the stats: What we mean by 'Completed'?: The files has been translated by a member of the localization team and peer-reviewed by an external person with expertise in computer science and Swahili.
Although the tools has been designed to satisfy our special needs at the Open Swahili Localization Project, we have put special effort in a clean design to allow other localization efforts to reuse and extend our code.
Special acknowledgement goes to Iñaki Cívico Campos for his C#, VB .NET work with ikakispelld and Louise Berthilson for her PHP work with Kipot, Kichapa and KamusiTZ.






Time to sleep. Buenas noches.

Copyright 2004 klnX Project, Creative Commons ShareAlike license: The licensor (Open Swahili Localization Project - also known as KiLiNuX or klnX) permits others to copy, distribute, display this work. In return, licensees must give the original author(s) credit. Derivative works must be licensed under the same terms as the original work.
Notice that Microsoft has never assigned a Locale ID for Swahili in other countries (i.e. there is not any assignation for Swahili in Tanzania). The language IDs page is here.