Mradi wa Kuswahilisha Programu Huria (Kilinux) una furaha kutangaza uzinduzi rasmi wa Jambo OpenOffice.org utakaofanyika tarehe 28 Februari 2005. Uzinduzi rasmi wa toleo la Win32 la Jambo OpenOffice utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Dar es Salaam (Tanzania).
Tukio hilo litahudhuriwa na balozi Tolvald Akesson (Balozi wa Sweden, Tanzania) na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Frederick Sumaye na Mhe. Pius Ng'wandu (Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu).
Uzinduzi Rasmi wa Jambo OpenOffice.org
Mahali: Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Dar es Salaam
Tarehe: Februari 28, 2005
Muda: 3:30 UM - 6:00 MU
Kiingilio: Bure