June 22, 2006 12:12 PM

Jambo Mozilla Firefox Tayari kwa Kupakua


Timu ya kilinux inayofuraha kuwatangaza kuwa Jambo Mozilla Firefox 1.o.3,
toleo la Kiswahili la Mozilla Firefox 1.0.3, ipo tayari kwa mapakuzi. Programu hii
inapatikana katika matoleo mawili; moja kwa ajili ya kompyuta zenye na mfumo wa
Windows XP na jingine kwa ajili ya kompyuta za Linux. Kupakua jambo Mozilla Firefox
nenda kwenye kipengele cha mapakuzi (kwenye tovuti hii) na chagua Pata Mozilla Firefox.


Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: FIREFOX, HABARI

June 14, 2005 3:42 PM

Uundaji wa Firefox katika Lugha ya Kiswahili Unaendelea


Timu ya klnX ipo mbioni kukamilisha uswahilishaji wa firefox-1.0.3.
Timu ina furaha kutangaza uundaji wa kwanza wa kivinjari webu cha firefox kwa Kiswahili.
Bado tunaendelea kuiboresha programu hii na kuondoa hitilafu ndogondogo ambazo zimejitokeza.
Pongezi kubwa kwa wana klnX wote.Toleo la kwanza la firefox limeundwa kati ya tarehe 10 na 14 Juni 2005 katika Idara ya Sayansi ya Kompyuta - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye maabara ya klnX.Imetumwa na Kennedy Frank | Kiungodumu | Kategoria: FIREFOX, HABARI

Machi 10, 2005 7:47 MU

Uswahilishaji wa Firefox umeanza


Baada ya kuzindua kwa mafanikio toleo letu la kwanza la kishwahili la OpenOffice.org 1.1.3 (Jambo OpenOffice.org 1.1.3) , Timu ya klnX imeanza uswahilishaji wa kivinjari huria kinachoitwa Firefox 1.0.3

Sauti ya Timu ya klnX.......


Imetumwa na Kennedy Frank | Kiungodumu | Kategoria: FIREFOX