Machi 10, 2005 7:47 MU

Uswahilishaji wa Firefox umeanza


Baada ya kuzindua kwa mafanikio toleo letu la kwanza la kishwahili la OpenOffice.org 1.1.3 (Jambo OpenOffice.org 1.1.3) , Timu ya klnX imeanza uswahilishaji wa kivinjari huria kinachoitwa Firefox 1.0.3

Sauti ya Timu ya klnX.......


Imetumwa na Kennedy Frank | Kiungodumu | Kategoria: FIREFOX

Februari 20, 2005 5:41 UM

Uzinduzi Rasmi wa Jambo OpenOffice


Mradi wa Kuswahilisha Programu Huria (Kilinux) una furaha kutangaza uzinduzi rasmi wa Jambo OpenOffice.org utakaofanyika tarehe 28 Februari 2005. Uzinduzi rasmi wa toleo la Win32 la Jambo OpenOffice utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Dar es Salaam (Tanzania).

Tukio hilo litahudhuriwa na balozi Tolvald Akesson (Balozi wa Sweden, Tanzania) na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Frederick Sumaye na Mhe. Pius Ng'wandu (Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu).

Uzinduzi Rasmi wa Jambo OpenOffice.org
Mahali: Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Dar es Salaam
Tarehe: Februari 28, 2005
Muda: 3:30 UM - 6:00 MU
Kiingilio: Bure


Imetumwa na Kennedy Frank | Kiungodumu | Kategoria: HABARI, OPENOFFICE, SWAHILI LOCALE

February 16, 2005 10:19 AM

Kilinux Software-MIRRORS NEEDED!


We are preparing the release of Jambo OpenOffice.org and need some mirrors (Specially in Tanzania and East Africa). The size of the software is as follows:

  • Jambo OpenOffice.org Win32 (Swahili)- 73MB
  • Jambo OpenOffice.org Linux (Swahili)- 81MB
  • Full Kilinux CD including TuxPaint and all English versionswith Swahili Spellchecker450M
  • Kilinux CD ISO-9960 450

Contact kenny@cs.udsm.ac.tz if you can offer some collocation space for the software.


Imetumwa na Kennedy Frank | Kiungodumu | Kategoria: HABARI