December 20, 2005 2:13 PM

Mafunzo ya Ujanibishaji yaliyofanyika Afrika Kusini


Timu ya kilinux ilihudhuria mafunzo ya ujanibishaji yaliyofanyika Afrika
ya Kusini kuanzia Novemba 28, 2005 hadi Desemba 2, 2005. Mafunzo haya
yaliandaliwa kwa pamoja na Translate.org.za (Mradi wa Ujanibishaji wa
Afrika Kusini) na Kilinux.udsm.ac.tz (Mradi wa Ujanibishaji wa Tanzania).

Madhumuni hasa ya mafunzo haya yalikuwa ni kutoa mafunzo kwa timu ya
Kilinux juu ya utaalamu wa kiufundi na kilugha unaohitajika kwa ajili
ya mchakato wa ujanibishaji. Mafunzo yaliongozwa na wafanyakazi
wa Translate.org.za.

Timu ya Kilinux ilijifunza mambo yafuatayo:

  • Zana za ujanibishaji
  • Mfumo Matoleo wa Sasa (CVS)
  • Uundaji OpenOffice.org.
  • Uendelezaji Farahasa
  • Ustahimili wa Miradi ya Ujanibishaji Programu Huria

Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: HABARI

December 15, 2005 3:31 PM

Kilele cha Mkutano wa Dunia wa Jamii ya Habari (Tunis, Tunisia Novemba 16-18, 2005)


Mradi wa Kilinux ulikua ni mojawapo ya miradi iliyoshiriki katika Kilele cha
Mkutano wa Dunia wa Jamii ya Habari (WSIS) uliofanyika Tunis, kuanzia
Novemba 16 hadi Novemba 18, 2005. Mkutano huo ulikusanya wawakilishi
kutoka miradi mbalimbali na waanzilishi wengineo kutoka duniani kote.

Mojawapo ya malengo ya Kilele hiki ni kuunda Jamii ya Habari madhubuti ili
watu kila mahali waweze kuunda, kufikia na kuchangia habari na maarifa ili
kufanikisha na kutimiza shabaha na malengo ya maendeleo yaliyokubaliwa.

Kilele hiki kinatazamwa kama msingi muhimu katika jitihada za dunia kuondoa
umaskini. Vilevile kimetoa utambuzi juu ya faida ambazo Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEKNOHAMA) inaweza ikaleta kwa jamii na jinsi ya
kubadilisha kazi, mawasiliano na maisha ya watu.

Kwa ukweli huo, mikutano na midahalo mingi ilifanyika ili kujadili na kuchangia
mawazo na maarifa kuhusu jinsi gani ya kufanikisha shabaha na malengo
yaliyokubaliwa. Mwakilishi wa Mradi wa Kilinux alipata nafasi ya kuwasilisha
mada juu ya kilinux na mchakato mzima wa ujanibishaji programu huria
Novemba 17 siku ambayo ilifahamika kama Siku ya Tanzania. Uwasilishaji
huo ulifuatiwa na maswali.

Kwenye banda la Tanzania programu ya Jambo OpenOffice na Jambo Mozilla
Firefox zilioneshwa, na watu wengi walivutiwa sana na programu hizi.
Baadhi ya watu waliovutiwa na klnX na wakapewa nakala ya CD ya
Jambo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Astrid Dufborg balozi wa
TEKNOHAMA kwa Sweden na mkuu wa ujumbe wa Sweden WSIS,
Mhe. Nandi-Ndaitwah waziri wa Habari na Utangazaji wa Namibia,
Mhe. Dk Ivy Matsepe-Casaburri waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini
na mabalozi wetu Ami Mpungwe na Mohammed Sheya na wengine wengi.

Picha za baadhi ya matukio zitakuwepo baada ya muda.


Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: HABARI

December 15, 2005 3:15 PM

Usajili wa Firefox


Sasa hivi tupo katika mchakato wa kusajili ili kupata akaunti ya CVS kwa ajili
ya ujanibishaji wa Firefox kutoka shirika la Mozilla. Hili litachukua siku kadhaa
kupata ufikio kwenye seva ya CVS.


Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: HABARI