June 14, 2005 3:42 PM

Uundaji wa Firefox katika Lugha ya Kiswahili Unaendelea

Timu ya klnX ipo mbioni kukamilisha uswahilishaji wa firefox-1.0.3.
Timu ina furaha kutangaza uundaji wa kwanza wa kivinjari webu cha firefox kwa Kiswahili.
Bado tunaendelea kuiboresha programu hii na kuondoa hitilafu ndogondogo ambazo zimejitokeza.
Pongezi kubwa kwa wana klnX wote.Toleo la kwanza la firefox limeundwa kati ya tarehe 10 na 14 Juni 2005 katika Idara ya Sayansi ya Kompyuta - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye maabara ya klnX.Imetumwa na Kennedy Frank | Kategoria: FIREFOX, HABARI