July 12, 2005 2:42 PM

Maonesho ya Jambo OpenOffice.org 1.1.3 (Bungeni - Dodoma, Juni 20-24, 2005)

Katika maonesho ya programu, machapisho na vitabu mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es salaam
yaliyofanyika Dodoma (Bungeni), Timu ya Kilinux ilipata fursa ya kuonesha
programu ya kwanza ya kiswahili iitwayo Jambo OpenOffice.org 1.1.3 ambayo humuwezesha
mtumiaji wa lugha ya Kiswahili kuunda maandiko, mawasilisho, michoro, kuunda tovuti n.k.

Katika Maonesho hayo waheshimiwa mawaziri na wabunge walikipongeza chuo kikuu cha
Dar es Salaam kupitia idara ya Sayansi ya Kompyuta kwa kuanzisha mradi wa Uswahilishaji
Programu Huria. Pia walichukua programu hiyo kwa wingi ili ikatumike maofisini na sehemu
nyinginezo nchini.


Imetumwa na Kennedy Frank | Kategoria: HABARI, OPENOFFICE