August 17, 2005 1:39 PM

Uhamishaji wa Jambo kutoka toleo 1.1.3 kwenda toleo 2.0

Timu ya klnX ipo mbioni kuanza uhamishaji wa Jambo OpenOffice kutoka toleo 1.1.3 kwenda toleo 2.0 kwa kushirikiana na Alberto Escudero kutoka it46 Global Consultancy.

Kulingana na mpangilio wa sasa wa kazi, mchakato wa uhamishaji unatarajiwa kukamilika Januari 2006. Timu imeshakusanya zana zote muhimu kwa ajili ya mchakato wa uhamishaji. Baada ya kuunganisha Jambo OpenOffice 1.1.3 na OpenOffice 2.0, tulipata jumla ya tungo 57844 kati ya hizo takribani tungo 20000 zimetafsiriwa.

Bado tunashughulikia kisakinishi cha firefox 1.0.3 kwa ajili ya Linux na Windows XP. Kisakinishi cha
Linux karibia kinakamilika ingawa majaribio yameonesha kuwa kimeshindwa kusakinisha katika baadhi ya kompyuta hivyo timu bado inaendelea kurekebisha tatizo hili.


Imetumwa na James Chambua | Kategoria: HABARI, OPENOFFICE