December 20, 2005 2:13 PM

Mafunzo ya Ujanibishaji yaliyofanyika Afrika Kusini

Timu ya kilinux ilihudhuria mafunzo ya ujanibishaji yaliyofanyika Afrika
ya Kusini kuanzia Novemba 28, 2005 hadi Desemba 2, 2005. Mafunzo haya
yaliandaliwa kwa pamoja na Translate.org.za (Mradi wa Ujanibishaji wa
Afrika Kusini) na Kilinux.udsm.ac.tz (Mradi wa Ujanibishaji wa Tanzania).

Madhumuni hasa ya mafunzo haya yalikuwa ni kutoa mafunzo kwa timu ya
Kilinux juu ya utaalamu wa kiufundi na kilugha unaohitajika kwa ajili
ya mchakato wa ujanibishaji. Mafunzo yaliongozwa na wafanyakazi
wa Translate.org.za.

Timu ya Kilinux ilijifunza mambo yafuatayo:

  • Zana za ujanibishaji
  • Mfumo Matoleo wa Sasa (CVS)
  • Uundaji OpenOffice.org.
  • Uendelezaji Farahasa
  • Ustahimili wa Miradi ya Ujanibishaji Programu Huria

Imetumwa na James Chambua | Kategoria: HABARI