Karibu kwenye tovuti ya Kilinux (klnX)!
klnX ni Mradi wa Kuswahilisha Programu ya Linux ulionzishwa na Idara ya Sayansi ya Kompyuta ikishirikiana na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). [Zaidi » ]

June 22, 2006 12:12 PM

Jambo Mozilla Firefox Tayari kwa Kupakua


Timu ya kilinux inayofuraha kuwatangaza kuwa Jambo Mozilla Firefox 1.o.3,
toleo la Kiswahili la Mozilla Firefox 1.0.3, ipo tayari kwa mapakuzi. Programu hii
inapatikana katika matoleo mawili; moja kwa ajili ya kompyuta zenye na mfumo wa
Windows XP na jingine kwa ajili ya kompyuta za Linux. Kupakua jambo Mozilla Firefox
nenda kwenye kipengele cha mapakuzi (kwenye tovuti hii) na chagua Pata Mozilla Firefox.


Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: FIREFOX, HABARI

May 15, 2006 3:47 PM

Washindi "Stockholm Challenge" 2006


Mradi wa KiLiNuX ulitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mashindano ya Stockholm 2006 baada ya kuwa mradi bora wa TEKNOHAMA katika kategoria ya Elimu kwenye mashindano hayo. Jumla ya miradi 172 kutoka mataifa mbalimbali ilichuana ambapo miradi 32 tu ndio ilifanikiwa kuingia fainali.

Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: HABARI

March 27, 2006 12:53 PM

Fainali ya Mashindano ya Stockholm 2006


Baraza la Mashindano la Stockholmlimeupitisha Mradi wa Kilinux kama moja ya miradi iliyoingia fainali katika kategoria ya Elimu kwa tuzo za mwaka huu za Mashindano ya Stockholm.
Miradi 148 imetangazwa kuwa imeingia fainali za mashindano hayo yenye kategoria sita ambazo ni Utamaduni, Maendeleo ya Uchumi, Elimu, Mazingira, Afya na Utawala wa umma.
Mshindi wa kila Kategoria atatangazwa wakati wa maadhimisho ya kukabidhi zawadi jijini Stockholm Mei 11.

Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: HABARI

December 20, 2005 2:13 PM

Mafunzo ya Ujanibishaji yaliyofanyika Afrika Kusini


Timu ya kilinux ilihudhuria mafunzo ya ujanibishaji yaliyofanyika Afrika
ya Kusini kuanzia Novemba 28, 2005 hadi Desemba 2, 2005. Mafunzo haya
yaliandaliwa kwa pamoja na Translate.org.za (Mradi wa Ujanibishaji wa
Afrika Kusini) na Kilinux.udsm.ac.tz (Mradi wa Ujanibishaji wa Tanzania).

Madhumuni hasa ya mafunzo haya yalikuwa ni kutoa mafunzo kwa timu ya
Kilinux juu ya utaalamu wa kiufundi na kilugha unaohitajika kwa ajili
ya mchakato wa ujanibishaji. Mafunzo yaliongozwa na wafanyakazi
wa Translate.org.za.

Timu ya Kilinux ilijifunza mambo yafuatayo:

  • Zana za ujanibishaji
  • Mfumo Matoleo wa Sasa (CVS)
  • Uundaji OpenOffice.org.
  • Uendelezaji Farahasa
  • Ustahimili wa Miradi ya Ujanibishaji Programu Huria

Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: HABARI

December 15, 2005 3:31 PM

Kilele cha Mkutano wa Dunia wa Jamii ya Habari (Tunis, Tunisia Novemba 16-18, 2005)


Mradi wa Kilinux ulikua ni mojawapo ya miradi iliyoshiriki katika Kilele cha
Mkutano wa Dunia wa Jamii ya Habari (WSIS) uliofanyika Tunis, kuanzia
Novemba 16 hadi Novemba 18, 2005. Mkutano huo ulikusanya wawakilishi
kutoka miradi mbalimbali na waanzilishi wengineo kutoka duniani kote.

Mojawapo ya malengo ya Kilele hiki ni kuunda Jamii ya Habari madhubuti ili
watu kila mahali waweze kuunda, kufikia na kuchangia habari na maarifa ili
kufanikisha na kutimiza shabaha na malengo ya maendeleo yaliyokubaliwa.

Kilele hiki kinatazamwa kama msingi muhimu katika jitihada za dunia kuondoa
umaskini. Vilevile kimetoa utambuzi juu ya faida ambazo Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEKNOHAMA) inaweza ikaleta kwa jamii na jinsi ya
kubadilisha kazi, mawasiliano na maisha ya watu.

Kwa ukweli huo, mikutano na midahalo mingi ilifanyika ili kujadili na kuchangia
mawazo na maarifa kuhusu jinsi gani ya kufanikisha shabaha na malengo
yaliyokubaliwa. Mwakilishi wa Mradi wa Kilinux alipata nafasi ya kuwasilisha
mada juu ya kilinux na mchakato mzima wa ujanibishaji programu huria
Novemba 17 siku ambayo ilifahamika kama Siku ya Tanzania. Uwasilishaji
huo ulifuatiwa na maswali.

Kwenye banda la Tanzania programu ya Jambo OpenOffice na Jambo Mozilla
Firefox zilioneshwa, na watu wengi walivutiwa sana na programu hizi.
Baadhi ya watu waliovutiwa na klnX na wakapewa nakala ya CD ya
Jambo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Astrid Dufborg balozi wa
TEKNOHAMA kwa Sweden na mkuu wa ujumbe wa Sweden WSIS,
Mhe. Nandi-Ndaitwah waziri wa Habari na Utangazaji wa Namibia,
Mhe. Dk Ivy Matsepe-Casaburri waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini
na mabalozi wetu Ami Mpungwe na Mohammed Sheya na wengine wengi.

Picha za baadhi ya matukio zitakuwepo baada ya muda.


Imetumwa na James Chambua | Kiungodumu | Kategoria: HABARI